Amos 4:10
“Niliwapelekea tauni miongoni mwenu 2 kama nilivyofanya kule Misri. 1 Niliwaua vijana wenu wa kiume kwa upanga, 2 niliwachukua farasi wenu. 1 Nilijaza pua zenu kwa uvundo kutoka kwenye kambi zenu, 2 hata hivyo hamjanirudia mimi,” 4 asema Bwana. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 9:3mkono wa Bwana utaleta pigo baya kwa mifugo yako, juu ya farasi wako, punda, ngamia, ngʼombe wako, kondoo na mbuzi.
Exodus 9:17Bado unaendelea kujiinua juu ya watu wangu, wala hutaki kuwaachia waende.
Exodus 10:3Kwa hiyo Mose na Aroni wakaenda kwa Farao na kumwambia, “Hili ndilo Bwana, Mungu wa Waebrania, asemalo: ‘Utaendelea hata lini kukataa kunyenyekea mbele yangu? Waachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu.
Exodus 12:29Ilipofika usiku wa manane, Bwana akawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika Misri, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa Farao, mrithi wa kiti cha ufalme, hadi mzaliwa wa kwanza wa mfungwa, aliyekuwa gerezani, na wazaliwa wa kwanza wa mifugo yote pia.
Exodus 15:26Mungu akasema, “Kama mkisikiliza kwa bidii sauti ya Bwana Mungu wenu na kuyafanya yaliyo sawa machoni pake, kama mkiyatii maagizo yake na kuzishika amri zake zote, sitaleta juu yenu ugonjwa wowote niliowaletea Wamisri, kwa kuwa Mimi ndimi Bwana, niwaponyaye.”
Leviticus 26:25Nitawaletea upanga juu yenu ili kuwapatiliza kwa kuvunja Agano langu. Mtakapokimbilia mijini mwenu, nitatuma tauni katikati yenu, nanyi mtatiwa mikononi mwa adui zenu.