Amos 4:6
“Niliwapa njaa kwenye kila mji, 2 na ukosefu wa chakula katika kila mji, 2 hata hivyo bado hamjanirudia mimi,” 4 asema Bwana. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Leviticus 26:26Nitakapowaondolea upatikanaji wa mkate wenu, wanawake kumi wataoka mkate wenu katika tanuru moja, nao wataugawa mkate kidogo kwa kupima. Mtakula, lakini hamtashiba.
Ruth 1:1Wakati Waamuzi walipotawala Israeli, kulikuwa na njaa katika nchi. Mtu mmoja kutoka nchi ya Bethlehemu ya Yuda, pamoja na mke wake na wanawe wawili, akaenda kuishi katika nchi ya Moabu.
1 Kings 18:2Kwa hiyo Eliya akaenda kujionyesha kwa Ahabu. Wakati huu njaa ilikuwa kali sana katika Samaria,
2 Kings 6:25Kukawa na njaa kuu katika mji. Samaria ilizingirwa kwa muda mrefu, kiasi kwamba kichwa cha punda kiliuzwa kwa shekeli themanini + 6:25 Shekeli 80 za fedha ni sawa na kilo moja. za fedha, na robo ya kibaba + 6:25 Robo ya kibaba ni sawa na lita 0.3. cha mavi ya njiwa kiliuzwa kwa shekeli tano + 6:25 Shekeli tano za fedha ni sawa na gramu 55. za fedha.
2 Chronicles 28:22Katika wakati wake wa mateso Mfalme Ahazi akazidi kukosa uaminifu kwa Bwana.
Isaiah 9:12Waashuru kutoka upande wa mashariki 2 na Wafilisti kutoka upande wa magharibi 2 wameila Israeli kwa kinywa kilichopanuliwa. 1 Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali, 2 mkono wake bado umeinuliwa juu. 1