Daniel 11:45
Atasimika hema zake za ufalme kati ya bahari na mlima mtakatifu wa kupendeza. Hata hivyo, atafikia mwisho wake, wala hakuna yeyote atakayemsaidia.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Numbers 34:5mahali ambapo utapinda, na kuunganika na Kijito cha Misri na kumalizikia kwenye Bahari ya Kati. + 34:5 Yaani Mediterania.
Isaiah 2:2Katika siku za mwisho 1 mlima wa Hekalu la Bwana utaimarishwa 2 kama mlima mkuu miongoni mwa milima yote, 1 utainuliwa juu ya vilima, 2 na mataifa yote yatamiminika huko.
Isaiah 14:13Ulisema moyoni mwako, 2 “Nitapanda juu hadi mbinguni, 1 nitakiinua kiti changu cha enzi 2 juu ya nyota za Mungu, 1 nitaketi nimetawazwa 2 juu ya mlima wa kusanyiko, 2 kwenye vimo vya juu sana vya Mlima Mtakatifu. 1
Ezekiel 39:2Nitakugeuza kuelekea ulikotoka na kukuburuta. Nitakuleta kutoka kaskazini ya mbali na kukupeleka wewe dhidi ya milima ya Israeli.
Daniel 7:26“ ‘Lakini mahakama itakaa kuhukumu, nayo mamlaka yake yataondolewa na kuangamizwa kabisa milele.
Daniel 11:16Huyo mvamia nchi atafanya apendavyo; hakuna yeyote atakayeweza kumpinga. Atajiimarisha katika Nchi ya Kupendeza, na atakuwa na uwezo wa kuiangamiza.