Daniel 8:4
Nikamtazama yule kondoo dume alivyokuwa akishambulia kuelekea magharibi, kaskazini na kusini. Hakuna mnyama yeyote aliyeweza kusimama dhidi yake, wala hakuna aliyeweza kuokoa kutoka nguvu zake. Alifanya kama atakavyo, naye akawa mkuu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Job 10:7ingawa wajua kuwa mimi sina hatia, 2 na hakuna awezaye kunitoa mkononi mwako? 1
Psalms 50:22“Yatafakarini haya, ninyi mnaomsahau Mungu, 2 ama sivyo nitawararua vipande vipande, 2 wala hapatakuwepo na yeyote wa kuwaokoa: 1
Isaiah 45:1“Hili ndilo asemalo Bwana kwa mpakwa mafuta wake, 2 Koreshi, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume 1 kutiisha mataifa mbele yake 2 na kuwavua wafalme silaha zao, 1 kufungua milango mbele yake 2 ili malango yasije yakafungwa: 1
Jeremiah 50:1Hili ndilo neno alilosema Bwana kupitia nabii Yeremia kuhusu Babeli na nchi ya Wakaldayo: 1
Daniel 5:19Kwa sababu ya nafasi ya juu aliyompa baba yako, kabila zote za watu, mataifa na watu wa kila lugha walimhofu na kumwogopa. Wale ambao mfalme alitaka kuwaua, aliwaua; wale aliotaka kuwaacha hai, aliwaacha hai; wale aliotaka kuwapandisha cheo, aliwapandisha; aliotaka kuwashusha, aliwashusha.
Daniel 7:5“Hapo mbele yangu kulikuwa na mnyama wa pili, ambaye alionekana kama dubu. Upande wake mmoja ulikuwa umeinuka, na alikuwa na mbavu tatu katika kinywa chake kati ya meno yake. Akaambiwa, ‘Amka, ule nyama mpaka ushibe!’