Daniel 7:5
“Hapo mbele yangu kulikuwa na mnyama wa pili, ambaye alionekana kama dubu. Upande wake mmoja ulikuwa umeinuka, na alikuwa na mbavu tatu katika kinywa chake kati ya meno yake. Akaambiwa, ‘Amka, ule nyama mpaka ushibe!’
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
2 Kings 2:24Akageuka, akawatazama na kuwalaani kwa Jina la Bwana. Kisha dubu wawili wa kike wakatokea mwituni na kuwararua vijana arobaini na wawili miongoni mwao.
Isaiah 13:17Tazama, nitawachochea Wamedi dhidi yao, 2 ambao hawajali fedha 2 wala hawafurahii dhahabu. 1
Isaiah 56:9Njooni, enyi wanyama wote wa kondeni, 2 njooni mle, ninyi wanyama wote wa mwituni! 1
Ezekiel 39:17“Mwanadamu, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ita kila aina ya ndege na wanyama wote wa mwituni, waambie: ‘Kusanyikeni mje pamoja kutoka pande zote kwa ajili ya dhabihu ninayowaandalia, dhabihu kuu katika milima ya Israeli. Huko mtakula nyama na kunywa damu.
Daniel 5:28Peresi: Ufalme wako umegawanywa na kupewa Wamedi na Waajemi.”
Daniel 8:4Nikamtazama yule kondoo dume alivyokuwa akishambulia kuelekea magharibi, kaskazini na kusini. Hakuna mnyama yeyote aliyeweza kusimama dhidi yake, wala hakuna aliyeweza kuokoa kutoka nguvu zake. Alifanya kama atakavyo, naye akawa mkuu.