Daniel 9:26
Baada ya majuma sitini na mawili, Mpakwa Mafuta atakatiliwa mbali, wala hatabaki na kitu. Watu wa mtawala atakayekuja watauharibu mji pamoja na mahali patakatifu. Mwisho utakuja kama mafuriko: Vita vitaendelea mpaka mwisho, nao ukiwa umeamriwa.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Psalms 22:15Nguvu zangu zimekauka kama kigae, 2 ulimi wangu umegandamana 2 na kaakaa la kinywa changu, 1 kwa sababu umenilaza 2 katika mavumbi ya kifo. 1
Isaiah 28:2Tazama, Bwana anaye mmoja aliye na uwezo na nguvu. 2 Kama dhoruba ya mvua ya mawe na upepo uharibuo, 1 kama mvua inyeshayo kwa nguvu na mafuriko yashukayo, 2 atakiangusha chini kwa nguvu. 1
Isaiah 53:8Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa. 2 Nani awezaye kueleza kuhusu kizazi chake? 1 Kwa maana alikatiliwa mbali na nchi ya walio hai, 2 alipigwa kwa ajili ya makosa ya watu wangu. 1
Daniel 9:27Mtawala huyo atathibitisha agano na watu wengi kwa juma moja. Katikati ya juma hilo atakomesha dhabihu na sadaka. Mahali pa dhabihu katika Hekalu atasimamisha chukizo la uharibifu, hadi mwisho ulioamriwa utakapomiminwa juu yake yeye aletaye uharibifu.”
Daniel 11:17Ataamua kuja na nguvu za ufalme wake wote na kufanya mapatano ya amani na mfalme wa Kusini. Naye atamtoa binti yake aolewe naye ili kuuangusha ufalme, lakini mipango yake haitafanikiwa wala kumsaidia.
Hosea 1:9Kisha Bwana akasema, “Mwite Lo-Ami + 1:9 Lo-Ami maana yake Sio watu wangu. kwa maana ninyi si watu wangu, nami si Mungu wenu.