Kumbukumbu 28:12
Bwana atafungua mbingu, ghala zake za baraka, kukupa mvua kwa majira yake na kubariki kazi zako zote za mikono yako. Utakopesha mataifa mengi lakini hutakopa kwa yeyote.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Leviticus 26:4nitawanyeshea mvua katika majira yake, nayo ardhi itatoa mazao yake, na miti ya mashambani itazaa matunda yake.
Deuteronomy 14:29ili Walawi (ambao hawana mashamba wala urithi wao wenyewe) na wageni, yatima na wajane wanaoishi kwenye miji yenu wapate kuja kula na kushiba, ili Bwana Mungu wenu apate kuwabariki ninyi katika kazi zote za mikono yenu.
Deuteronomy 15:10Mpe kwa ukarimu na ufanye hivyo bila kinyongo moyoni, ndipo kwa sababu ya hili Bwana Mungu wenu atakubariki katika kazi zako zote na kwa kila kitu utakachokiwekea mkono wako.
Deuteronomy 28:44Yeye atakukopesha, lakini wewe hutamkopesha. Yeye atakuwa kichwa, lakini wewe utakuwa mkia.
Psalms 65:9Waitunza nchi na kuinyeshea, 2 waitajirisha kwa wingi. 1 Vijito vya Mungu vimejaa maji 2 ili kuwapa watu nafaka, 2 kwa maana wewe umeviamuru. 1
Proverbs 22:7Matajiri huwatawala maskini 2 naye akopaye ni mtumwa wa akopeshaye. 1