Esta 3:15
Kwa kuharakishwa na amri ya mfalme, matarishi walikwenda na andiko lilitolewa katika mji wa ngome ya Shushani. Mfalme na Hamani waliketi na kunywa, lakini mji wa Shushani ulifadhaika.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 37:25Walipokaa ili wale chakula chao, wakainua macho wakaona msafara wa Waishmaeli ukija kutoka Gileadi. Ngamia wao walikuwa wamepakizwa mizigo ya vikolezo, uvumba na manemane, nao walikuwa njiani kuvipeleka Misri.
Esther 4:16“Nenda, kusanya pamoja Wayahudi wote walioko Shushani, nanyi mfunge kwa ajili yangu. Msile wala kunywa kwa siku tatu, usiku na mchana. Mimi na wajakazi wangu tutafunga kama mnavyofanya. Baada ya kufanyika hili, nitakwenda kwa mfalme, hata ingawa ni kinyume cha sheria. Ikiwa ni kuangamia na niangamie.”
Psalms 37:7Tulia mbele za Bwana 2 na umngojee kwa uvumilivu; 1 usisumbuke watu wanapofanikiwa katika njia zao, 2 wanapotekeleza mipango yao miovu. 1
Proverbs 4:16Kwa kuwa hawawezi kulala mpaka watende uovu; 2 wanashindwa hata kusinzia mpaka wamwangushe mtu. 1
Proverbs 31:4“Ee Lemueli, haifai wafalme, 2 haifai wafalme kunywa mvinyo, 2 haifai watawala kutamani sana kileo, 1
Amos 6:6Mnakunywa mvinyo kwa bakuli zilizojazwa, 2 na mnajipaka mafuta mazuri, 2 lakini hamhuzuniki kwa maangamizi ya Yosefu. 1