Kutoka 27:19
Vyombo vingine vyote vinavyotumika katika maskani kwa shughuli yoyote, pamoja na vigingi vyote na hata vile vya ua, vitakuwa vya shaba. 1 Mafuta Ya Kinara Cha Taa (Walawi 24:1-4)
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 27:3Tengeneza vyombo vyake vyote kwa shaba: vyungu vyake vya kuondolea majivu, masepetu, mabakuli ya kunyunyizia, uma za nyama, na vyombo vya kuchukulia moto.
Exodus 38:20Vigingi vyote vya maskani na vya ua ulioizunguka vilikuwa vya shaba. 1 Vifaa Vilivyotumika
Exodus 39:40mapazia ya ua pamoja na nguzo na vitako vyake, pia na pazia kwa ajili ya ingilio la kwenye ua; kamba zake na vigingi vya hema kwa ajili ya ua; vyombo vyote vilivyohitajiwa kwa ajili ya maskani, Hema la Kukutania;
Numbers 4:32nguzo za ua unaozunguka pamoja na vitako vyake, vigingi vya hema, kamba, vifaa vyake vyote na kila kitu kinachohusiana na matumizi yake. Kila mtu mpangie vitu maalum vya kubeba.
Ecclesiastes 12:11Maneno ya wenye hekima ni kama mchokoro, mithali zao zilizokusanywa pamoja ni kama misumari iliyogongomewa ikawa imara, yaliyotolewa na Mchungaji mmoja.
Isaiah 33:20Mtazame Sayuni, mji wa sikukuu zetu; 2 macho yenu yatauona Yerusalemu, 2 mahali pa amani pa kuishi, hema ambalo halitaondolewa, 1 nguzo zake hazitangʼolewa kamwe, 2 wala hakuna kamba yake yoyote itakayokatika. 1