Ezekiel 21:28
“Nawe, mwanadamu, tabiri na useme, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo kuhusu Waamoni na matukano yao. 1 “ ‘Upanga, upanga, 2 umefutwa kwa ajili ya kuua, 1 umesuguliwa ili kuangamiza 2 na unametameta kama umeme wa radi! 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
2 Chronicles 36:17Mungu akamwinua dhidi yao mfalme wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao wa kiume kwa upanga ndani ya mahali patakatifu, ambaye hakumbakiza kijana mwanaume wala kijana mwanamke, wazee wala vikongwe. Mungu akawatia wote mikononi mwa Nebukadneza.
Jeremiah 49:1Kuhusu Waamoni: Hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Je, Israeli hana wana? 2 Je, hana warithi? 1 Kwa nini basi Moleki amechukua milki ya Gadi? 2 Kwa nini watu wake wanaishi katika miji yake? 1
Ezekiel 17:15Lakini mfalme aliasi dhidi yake kwa kutuma wajumbe wake kwenda Misri ili kupatiwa farasi na jeshi kubwa. Je, atashinda? Je, atafanikiwa? Je, mtu afanyaye mambo kama hayo ataokoka? Je, atavunja mapatano na bado aokoke?
Ezekiel 21:20Weka alama njia moja kwa ajili ya upanga upate kuja dhidi ya Raba ya Waamoni na nyingine upate kuja dhidi ya Yuda na Yerusalemu iliyozungushiwa ngome.
Hosea 9:9Wamezama sana katika rushwa, 2 kama katika siku za Gibea. 1 Mungu atakumbuka uovu wao 2 na kuwaadhibu kwa ajili ya dhambi zao. 1
Zephaniah 2:8“Nimeyasikia matukano ya Moabu 2 nazo dhihaka za Waamoni, 1 ambao waliwatukana watu wangu 2 na kutoa vitisho dhidi ya nchi yao. 1