Ezekieli 39:7
“ ‘Nitalifanya Jina langu takatifu lijulikane miongoni mwa watu wangu Israeli. Sitaliacha tena Jina langu takatifu litiwe unajisi, nayo mataifa watajua kuwa Mimi Bwana ndimi Aliye Mtakatifu wa Israeli.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 20:7Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako, kwa kuwa Bwana hataacha kumhesabia hatia yeye alitajaye jina lake bure. 1
Isaiah 12:6Pazeni sauti mwimbe kwa furaha, watu wa Sayuni, 2 kwa maana mkuu ni yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli miongoni mwenu.”
Isaiah 43:14Hili ndilo Bwana asemalo, 2 Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli: 1 “Kwa ajili yenu nitatumana Babeli 2 na kuwaleta Wakaldayo wote kama wakimbizi, 2 katika meli walizozionea fahari. 1
Isaiah 60:9Hakika visiwa vinanitazama, 2 merikebu za Tarshishi + 60:9 Au: za biashara (ona pia 1Fal 10:22; 22:48; 2Nya 9:21; 20:36; Isa 2:16 ). ndizo zinazotangulia, 1 zikiwaleta wana wenu kutoka mbali, 2 wakiwa na fedha na dhahabu zao, 1 kwa heshima ya Bwana, Mungu wenu, 2 yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, 2 kwa maana amekujalia utukufu. 1
Ezekiel 20:9Lakini kwa ajili ya Jina langu nilifanya kile ambacho kingelifanya lisitiwe unajisi machoni mwa mataifa waliyoishi miongoni mwao na ambao machoni pao nilikuwa nimejifunua kwa Waisraeli kwa kuwatoa katika nchi ya Misri.
Ezekiel 20:39“ ‘Kwa habari zenu ninyi, ee nyumba ya Israeli, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nendeni mkatumikie sanamu zenu, kila mmoja wenu! Lakini baadaye hakika mtanisikiliza mimi nanyi hamtalinajisi tena Jina langu takatifu, kwa matoleo yenu na sanamu zenu.