Ezra 8:28
Niliwaambia, “Ninyi pamoja na vyombo hivi ni wakfu kwa Bwana. Fedha na dhahabu ni sadaka ya hiari kwa Bwana, Mungu wa baba zenu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Leviticus 21:6Lazima wawe watakatifu kwa Mungu wao, na kamwe wasilinajisi jina la Mungu wao. Kwa sababu ndio wanaotoa sadaka za kuteketezwa kwa moto kwa Bwana, chakula cha Mungu wao, hivyo lazima wawe watakatifu.
Numbers 4:4“Hii ndiyo kazi ya Wakohathi katika Hema la Kukutania: Watatunza vitu vilivyo vitakatifu sana.
Numbers 7:13Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, + 7:13 Shekeli 130 za fedha ni sawa na kilo 1.5. na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, + 7:13 Shekeli 70 za fedha ni sawa gramu 800. vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;
Deuteronomy 33:8Kuhusu Lawi alisema: 1 “Thumimu yako na Urimu + 33:8 Thumimu na Urimu maana yake Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha kifuani cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha. yako ulimpa, 2 mtu yule uliyemfadhili. 1 Ulimjaribu huko Masa 2 na kushindana naye 2 kwenye maji ya Meriba. 1
1 Chronicles 23:28Wajibu wa Walawi ulikuwa kuwasaidia wazao wa Aroni kuhudumu katika Hekalu la Bwana: Kuwa wasimamizi wa nyua, vyumba vya pembeni, kutakasa vyombo vitakatifu na utendaji mwingine wowote katika nyumba ya Mungu.
2 Chronicles 24:14Walipokamilisha kazi hiyo ya kukarabati, wakaleta fedha zilizobaki wakampa mfalme na Yehoyada, nao kwa hizo wakatengeneza vyombo kwa ajili ya Hekalu la Bwana: Vyombo kwa ajili ya huduma na kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, pia mabakuli na vitu vingine vya dhahabu na fedha. Wakati wote Yehoyada alipokuwa hai, sadaka za kuteketezwa zilitolewa wakati wote katika Hekalu la Bwana.