Genesis 22:17
hakika nitakubariki, na nitauzidisha uzao wako kama nyota za angani na kama mchanga ulioko pwani. Wazao wako watamiliki miji ya adui zao,
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
18na kupitia uzao wako mataifa yote duniani yatabarikiwa, kwa sababu umenitii.”
Cross References
Genesis 13:16Nitaufanya uzao wako uwe mwingi kama mavumbi ya nchi, hivyo kama kuna yeyote awezaye kuhesabu mavumbi, basi uzao wako utahesabika.
Genesis 17:6Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, kwako yatatoka mataifa nao wafalme watatoka kwako.
Genesis 26:4Nitafanya wazao wako kuwa wengi kama nyota za angani, nami nitawapa nchi hizi zote na kutokana na uzao wako mataifa yote yatabarikiwa,
Genesis 27:29Mataifa na yakutumikie 2 na mataifa yakusujudie. 1 Uwe bwana juu ya ndugu zako, 2 na wana wa mama yako wakusujudie. 1 Walaaniwe wale wakulaanio, 2 nao wale wakubarikio wabarikiwe.”
Genesis 28:14Uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi na mashariki, kaskazini na kusini. Kupitia wewe na uzao wako mataifa yote ya duniani yatabarikiwa.
Genesis 32:13Akalala pale usiku ule, miongoni mwa vitu alivyokuwa navyo, akachagua zawadi kwa ajili ya Esau ndugu yake: