Isaya 1:11
Bwana anasema, “Wingi wa sadaka zenu, 2 ni kitu gani kwangu? 1 Ninazo sadaka za kuteketezwa nyingi kupita kiasi, 2 za kondoo dume na mafuta ya wanyama walionona. 1 Sipendezwi na damu za mafahali 2 wala za wana-kondoo na mbuzi. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Psalms 50:8Sikukemei kwa sababu ya dhabihu zako, 2 au sadaka zako za kuteketezwa, 2 ambazo daima ziko mbele zangu. 1
Proverbs 15:8Bwana huchukia sana dhabihu za waovu, 2 bali maombi ya wanyofu humfurahisha Mungu. 1
Isaiah 66:3Lakini yeyote atoaye dhabihu ya fahali 2 ni kama yeye auaye mtu, 1 na yeyote atoaye sadaka ya mwana-kondoo, 2 ni kama yule avunjaye shingo ya mbwa. 1 Yeyote atoaye sadaka ya nafaka, 2 ni kama yule aletaye damu ya nguruwe, 1 na yeyote afukizaye uvumba wa kumbukumbu, 2 ni kama yule aabuduye sanamu. 1 Wamejichagulia njia zao wenyewe, 2 nazo nafsi zao zinafurahia machukizo yao. 1
Jeremiah 7:21“ ‘Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Endeleeni, ongezeni sadaka zenu za kuteketezwa juu ya dhabihu zenu nyingine, mle nyama hiyo wenyewe!
Amos 4:5Mchome mkate uliotiwa chachu kama sadaka ya shukrani, 2 jisifuni kuhusu sadaka zenu za hiari: 1 jigambeni kwa ajili ya sadaka hizo, enyi Waisraeli, 2 kwa kuwa hili ndilo mnalopenda kulitenda,” 4 asema Bwana Mwenyezi. 1
Micah 6:7Je, Bwana atafurahishwa na kondoo dume elfu, 2 au mito elfu kumi ya mafuta? 1 Je, nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa ajili ya kosa langu, 2 mtoto wangu mwenyewe 2 kwa ajili ya dhambi ya nafsi yangu? 1