Isaiah 14:3
Katika siku Bwana atakapokuondolea mateso, udhia na utumwa wa kikatili,
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Deuteronomy 28:65Miongoni mwa mataifa hayo hamtapata raha wala mahali pa kupumzisha wayo wa mguu wenu. Huko Bwana atawapa mahangaiko ya mawazo, macho yaliyochoka kwa kungojea na moyo uliokata tamaa.
Isaiah 11:10Katika siku hiyo, Shina la Yese atasimama kama bendera kwa ajili ya mataifa. Mataifa yatakusanyika kwake, na mahali pake pa kupumzikia patakuwa utukufu.
Isaiah 32:18Watu wangu wataishi katika makao ya mahali pa amani, 2 katika nyumba zilizo salama, 2 katika mahali pa kupumzika pasipo na usumbufu. 1
Jeremiah 30:8“ ‘Katika siku ile,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote, 2 ‘nitaivunja nira kutoka shingoni mwao 1 na kuvipasua vifungo vyao; 2 wageni hawatawafanya tena watumwa. 1
Jeremiah 46:27“Usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu, 2 usifadhaike, ee Israeli. 1 Hakika nitakuokoa kutoka nchi za mbali, 2 uzao wako kutoka nchi ya uhamisho wao. 1 Yakobo atakuwa tena na amani na salama, 2 wala hakuna hata mmoja atakayewatia hofu. 1
Ezekiel 28:24“ ‘Nyumba ya Israeli hawatakuwa tena na majirani wenye nia ya kuwadhuru wanaoumiza kama michongoma na miiba mikali. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana Mwenyezi.