Kumbukumbu 28:65
Miongoni mwa mataifa hayo hamtapata raha wala mahali pa kupumzisha wayo wa mguu wenu. Huko Bwana atawapa mahangaiko ya mawazo, macho yaliyochoka kwa kungojea na moyo uliokata tamaa.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 8:9Lakini hua hakupata mahali pa kutua kwa kuwa maji yalienea juu ya uso wa dunia yote, kwa hiyo akarudi kwa Noa ndani ya safina. Noa akanyoosha mkono akamchukua yule hua akamrudisha ndani ya safina.
Leviticus 26:36“ ‘Kwa habari ya wenzenu wale watakaobaki, nitaifanya mioyo yao kuwa na hofu kuu katika nchi za adui zao, kiasi kwamba sauti ya jani linalopeperushwa na upepo itawafanya wakimbie. Watakimbia kana kwamba wanakimbia upanga, nao wataanguka, ingawa hakuna anayewafukuza.
Isaiah 57:21Mungu wangu asema, 2 “Hakuna amani kwa waovu.”
Lamentations 1:3Baada ya mateso na kufanyishwa kazi kikatili, 2 Yuda amekwenda uhamishoni. 1 Anakaa miongoni mwa mataifa, 2 hapati mahali pa kupumzika. 1 Wote ambao wanamsaka wamemkamata 2 katikati ya dhiki yake. 1
Lamentations 5:17Kwa sababu hiyo, mioyo yetu inazimia, 2 kwa sababu ya hayo, macho yetu yamefifia, 1
Ezekiel 12:18“Mwanadamu, tetemeka wakati ulapo chakula chako, tetemeka kwa hofu wakati unywapo maji yako.