Isaiah 17:7
Katika siku ile watu watamwangalia Muumba wao, 2 na kuelekeza macho yao kwa yule Aliye Mtakatifu wa Israeli. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
2 Chronicles 30:10Matarishi wakaenda mji hadi mji katika Efraimu na Manase, wakafika mpaka Zabuloni, lakini watu wakawadharau na kuwadhihaki.
2 Chronicles 31:1Baada ya mambo haya yote kumalizika, Waisraeli ambao walikuwako huko wakaenda kwenye miji ya Yuda, wakayavunja yale mawe ya kuabudia na kuzikatakata zile nguzo za Ashera. Wakabomoa mahali pa juu pa kuabudia miungu pamoja na madhabahu zake kila mahali katika Yuda na Benyamini na katika Efraimu na Manase. Baada ya kuviharibu hivi vyote, Waisraeli wakarudi katika miji yao wenyewe na kwenye milki zao.
Isaiah 10:20Katika siku ile, mabaki ya Israeli, 2 walionusurika wa nyumba ya Yakobo, 1 hawatamtegemea tena yeye aliyewapiga, 2 lakini watamtegemea kwa kweli 2 Bwana Aliye Mtakatifu wa Israeli. 1
Isaiah 22:11Mlijenga bwawa la maji katikati ya kuta mbili 2 kwa ajili ya maji ya Bwawa la Zamani, 1 lakini hamkumtazama Yule aliyelitengeneza, 2 au kuwa na heshima kwa Yule aliyeubuni tangu zamani za kale. 1
Isaiah 29:18Katika siku ile viziwi watasikia maneno ya kitabu, 2 na katika utusitusi na giza 2 macho ya kipofu yataona. 1
Jeremiah 3:12Nenda, ukatangaze ujumbe huu kuelekea kaskazini: 1 “ ‘Rudi, Israeli usiye mwaminifu,’ asema Bwana, 2 ‘sitakutazama tena kwa uso uliokunjamana, 1 kwa kuwa mimi ni mwenye huruma,’ asema Bwana, 2 ‘Sitashika hasira yangu milele. 1