Isaiah 19:3
Wamisri watakufa moyo, 2 na nitaibatilisha mipango yao. 1 Watatafuta ushauri kwa sanamu na kwa roho za waliokufa, 2 kwa waaguzi na kwa wale waongeao na mizimu. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
1 Samuel 25:37Basi asubuhi, Nabali alipokuwa amelevuka, mkewe akamwambia mambo yote, nao moyo wake ukazimia, akawa kama jiwe.
2 Samuel 17:14Absalomu na watu wote wa Israeli wakasema, “Shauri la Hushai, Mwariki, ni jema zaidi kuliko lile la Ahithofeli.” Kwa maana Bwana alikuwa amekusudia kupinga shauri nzuri la Ahithofeli, ili kuleta maafa juu ya Absalomu.
2 Kings 1:2Basi Ahazia alikuwa ameanguka huko Samaria kutoka baraza ya chumba chake cha juu, akaumia. Hivyo akatuma wajumbe, akiwaambia, “Nendeni mkaulize kwa Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni, mkaone kama nitapona kutokana na kuumia huku.”
2 Chronicles 25:16Wakati nabii alipokuwa angali anazungumza, mfalme akamwambia, “Je, wewe tumekuchagua kuwa mshauri wa mfalme? Nyamaza, ya nini uuawe?” Hivyo nabii akanyamaza lakini akasema, “Najua kuwa Mungu ameazimia kukuangamiza kwa sababu umefanya jambo hili na hukusikiliza shauri langu.”
Job 5:13Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao, 2 nayo mipango ya wadanganyifu huifagilia mbali. 1
Psalms 107:27Walipepesuka na kuyumbayumba kama walevi, 2 ujanja wao ukafikia ukomo. 1