Isaya 23:18
Lakini faida na mapato yake yatawekwa wakfu kwa Bwana; hayatahifadhiwa wala kufichwa. Faida zake zitakwenda kwa wale wakaao mbele za Bwana kwa ajili ya chakula tele na mavazi mazuri.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 28:36“Tengeneza bamba la dhahabu safi na uchore juu yake maneno haya kama vile muhuri huchorwa: Mtakatifu kwa Bwana.
Deuteronomy 26:12Wakati utakapokuwa umeshatoa zaka zote za mazao yako katika mwaka wa tatu, ambao ni mwaka wa zaka, utampa Mlawi, mgeni, yatima na mjane, ili waweze kula katika miji yenu na kushiba.
2 Chronicles 2:11Ndipo Hiramu mfalme wa Tiro akamjibu Solomoni kwa barua: “Kwa sababu Bwana anawapenda watu wake, amekufanya wewe kuwa mfalme wao.”
Psalms 72:10Wafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbali 2 watamletea kodi; 1 wafalme wa Sheba na Seba 2 watampa zawadi. 1
Proverbs 13:22Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi, 2 bali mali ya wenye dhambi imehifadhiwa 2 kwa ajili ya wenye haki. 1
Ecclesiastes 2:26Kwa yule mtu anayempendeza Mungu, Mungu humpa hekima, maarifa na furaha, bali kwa mwenye dhambi Mungu humpa kazi ya kukusanya na kuhifadhi utajiri ili Mungu ampe yule anayempenda. Hili nalo pia ni ubatili, ni kukimbiza upepo.