Isaya 30:10
Wanawaambia waonaji, 2 “Msione maono tena!” 1 Nako kwa manabii wanasema, 2 “Msiendelee kutupatia maono 2 ambayo ni ya kweli! 1 Tuambieni mambo ya kupendeza, 2 tabirini mambo ya uongo. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
9Hawa ni watu waasi, watoto wadanganyifu, 2 watoto ambao hawataki kusikiliza mafundisho ya Bwana. 1
Cross References
1 Kings 21:20Ahabu akamwambia Eliya, “Kwa hiyo umenipata, wewe adui yangu!” Akajibu, “Ndiyo, nimekupata. Kwa sababu umejiuza mwenyewe kufanya uovu mbele ya macho ya Bwana.
1 Kings 22:13Mjumbe aliyekuwa amekwenda kumwita Mikaya akamwambia, “Tazama, manabii wote kama mtu mmoja wanatabiri ushindi kwa mfalme. Neno lako na likubaliane na lao, nawe unene mema kuhusu mfalme.”
2 Chronicles 16:10Asa akamkasirikia mwonaji kwa sababu ya jambo hili. Alikuwa ameghadhibika sana hata akamweka gerezani. Wakati huo huo Asa akaanza kuwatesa na kuwaonea baadhi ya watu kwa ukatili.
2 Chronicles 24:19Ingawa Bwana aliwatuma manabii wawarudishe watu kwake na ingawa waliwaonya, hawakuwasikiliza.
Job 41:3Je, ataendelea kukuomba umhurumie? 2 Atasema nawe maneno ya upole? 1
Jeremiah 5:31Manabii wanatabiri uongo, 2 makuhani wanatawala kwa mamlaka yao wenyewe, 1 nao watu wangu wanapenda hivyo. 2 Lakini mtafanya nini mwisho wake?