Isaiah 49:12
Tazama, watakuja kutoka mbali: 2 wengine kutoka kaskazini, wengine kutoka magharibi, 2 wengine kutoka nchi ya Sinimu.” + 49:12 Sinimu hapa ina maana ya Aswani. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
11Nitaifanya milima yangu yote kuwa barabara, 2 na njia kuu zangu zitainuliwa. 1
Cross References
Psalms 22:27Miisho yote ya dunia itakumbuka 2 na kumgeukia Bwana, 1 nazo jamaa zote za mataifa 2 watasujudu mbele zake, 1
Psalms 72:17Jina lake na lidumu milele, 2 na lidumu kama jua. 1 Mataifa yote yatabarikiwa kupitia kwake, 2 nao watamwita aliyebarikiwa. 1
Isaiah 11:10Katika siku hiyo, Shina la Yese atasimama kama bendera kwa ajili ya mataifa. Mataifa yatakusanyika kwake, na mahali pake pa kupumzikia patakuwa utukufu.
Isaiah 11:12Atainua bendera kwa mataifa 2 na kuwakusanya Waisraeli walioko uhamishoni; 1 atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika 2 kutoka pembe nne za dunia. 1
Isaiah 43:6Nitaiambia kaskazini, ‘Watoe!’ 2 nayo kusini, ‘Usiwazuie.’ 1 Walete wana wangu kutoka mbali, 2 na binti zangu kutoka miisho ya dunia: 1
Isaiah 66:19“Nitaweka ishara katikati yao, nami nitapeleka baadhi ya hao walionusurika kwa mataifa, hadi Tarshishi, kwa Puli + 66:19 Puli hapa inamaanisha Libya. na Waludi (wanaojulikana kama wapiga upinde), kwa Tubali na Uyunani, hadi visiwa vya mbali ambavyo havijasikia juu ya sifa zangu au kuuona utukufu wangu. Watatangaza utukufu wangu miongoni mwa mataifa.