Isaya 53:11
Baada ya maumivu ya nafsi yake, 2 ataona nuru ya uzima na kuridhika; 1 kwa maarifa yake, mtumishi wangu mwenye haki 2 atawafanya wengi kuwa wenye haki, 2 naye atayachukua maovu yao. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Isaiah 42:1“Huyu hapa mtumishi wangu, ninayemtegemeza, 2 mteule wangu, ambaye ninapendezwa naye; 1 nitaweka Roho yangu juu yake, 2 naye ataleta haki kwa mataifa. 1
Isaiah 49:3Akaniambia, “Wewe u mtumishi wangu, 2 Israeli, ambaye katika yeye 2 nitaonyesha utukufu wangu.” 1
Isaiah 53:8Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa. 2 Nani awezaye kueleza kuhusu kizazi chake? 1 Kwa maana alikatiliwa mbali na nchi ya walio hai, 2 alipigwa kwa ajili ya makosa ya watu wangu. 1
Daniel 9:24“Majuma sabini yameamriwa kwa ajili ya watu wako na kwa ajili ya mji wako mtakatifu, ili kumaliza makosa, kukomesha dhambi, kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, kuleta haki ya milele, kutia muhuri maono na unabii, na pia kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu sana.
Luke 22:44Naye akiwa katika maumivu makuu, akaomba kwa bidii, nalo jasho lake likawa kama matone ya damu yakidondoka ardhini.
John 12:24Amin, amin nawaambia, mbegu ya ngano isipoanguka ardhini na kufa, hubakia kama mbegu peke yake. Lakini ikifa huzaa mbegu nyingi.