Isaya 53:6
Sisi sote, kama kondoo, tumepotea, 2 kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe, 1 naye Bwana aliweka juu yake 2 maovu yetu sisi sote. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 22:6Abrahamu akachukua kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, akamtwika Isaki mwanawe, yeye mwenyewe akachukua moto na kisu. Walipokuwa wakienda pamoja,
Psalms 69:4Wale wanaonichukia bila sababu 2 ni wengi kuliko nywele za kichwa changu; 1 wengi ni adui kwangu bila sababu, 2 wale wanaotafuta kuniangamiza. 1 Ninalazimishwa kurudisha 2 kitu ambacho sikuiba. 1
Isaiah 53:10Lakini yalikuwa ni mapenzi ya Bwana 2 kumchubua na kumsababisha ateseke. 1 Ingawa Bwana amefanya maisha yake 2 kuwa sadaka ya hatia, 1 ataona uzao wake na kuishi siku nyingi, 2 nayo mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake. 1
Isaiah 56:11Ni mbwa wenye tamaa kubwa, 2 kamwe hawatosheki. 1 Wao ni wachungaji waliopungukiwa na ufahamu; 2 wote wamegeukia njia yao wenyewe, 2 kila mmoja hutafuta faida yake mwenyewe. 1
Jeremiah 50:6“Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea; 2 wachungaji wao wamewapotosha 1 na kuwasababisha kuzurura 2 juu ya milima. 1 Walitangatanga juu ya mlima na kilima, 2 na kusahau mahali pao wenyewe pa kupumzikia. 1
Matthew 18:12“Mwaonaje? Ikiwa mtu ana kondoo mia moja, na mmoja wao akapotea, je, hatawaacha wale tisini na tisa vilimani na kwenda kumtafuta huyo mmoja aliyepotea?