Isaya 57:6
“Sanamu zilizo katikati ya mawe laini ya mabondeni ndizo fungu lenu; 2 hizo ndizo sehemu yenu. 1 Naam, kwa hizo mmemimina sadaka za vinywaji, 2 na kutoa sadaka za nafaka. 1 Katika haya yote, 2 niendelee kuona huruma? 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
7Umeweka kitanda chako juu kwenye kilima kirefu kilichoinuka, 2 huko ulikwenda kutoa dhabihu zako. 1
Cross References
Deuteronomy 32:37Atasema: “Sasa iko wapi miungu yao, 2 mwamba walioukimbilia, 1
Isaiah 66:3Lakini yeyote atoaye dhabihu ya fahali 2 ni kama yeye auaye mtu, 1 na yeyote atoaye sadaka ya mwana-kondoo, 2 ni kama yule avunjaye shingo ya mbwa. 1 Yeyote atoaye sadaka ya nafaka, 2 ni kama yule aletaye damu ya nguruwe, 1 na yeyote afukizaye uvumba wa kumbukumbu, 2 ni kama yule aabuduye sanamu. 1 Wamejichagulia njia zao wenyewe, 2 nazo nafsi zao zinafurahia machukizo yao. 1
Jeremiah 5:9Je, nisiwaadhibu kwa ajili ya hili?” 2 asema Bwana. 1 “Je, nisijilipizie kisasi 2 juu ya taifa kama hili? 1
Jeremiah 7:18Watoto wanakusanya kuni, baba zao wanawasha moto, na wanawake wanakanda unga na kuoka mikate kwa ajili ya Malkia wa Mbinguni. Wanamimina sadaka za vinywaji kwa miungu mingine ili kunikasirisha.
Jeremiah 19:13Nyumba zilizoko Yerusalemu na zile za wafalme wa Yuda zitatiwa unajisi kama mahali hapa, Tofethi: yaani nyumba zote ambazo walifukiza uvumba juu ya mapaa yake kwa jeshi lote la angani, na kumimina dhabihu za vinywaji kwa miungu mingine.’ ”
Jeremiah 44:17Hakika tutafanya kila kitu tulichosema tutakifanya: Tutafukiza uvumba kwa Malkia wa Mbinguni na tutammiminia sadaka zetu za kinywaji kama vile sisi na baba zetu, wafalme wetu na maafisa wetu tulivyofanya katika miji ya Yuda na katika barabara za Yerusalemu. Wakati ule tulikuwa na chakula tele, tulikuwa matajiri wala hatukupata dhara lolote.