Yeremia 5:9
Je, nisiwaadhibu kwa ajili ya hili?” 2 asema Bwana. 1 “Je, nisijilipizie kisasi 2 juu ya taifa kama hili? 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Leviticus 26:25Nitawaletea upanga juu yenu ili kuwapatiliza kwa kuvunja Agano langu. Mtakapokimbilia mijini mwenu, nitatuma tauni katikati yenu, nanyi mtatiwa mikononi mwa adui zenu.
Deuteronomy 32:43Furahini, enyi mataifa, pamoja na watu wake, 2 kwa kuwa atailipiza damu ya watumishi wake, 1 atalipiza kisasi juu ya adui zake 2 na kufanya upatanisho 2 kwa ajili ya nchi na watu wake.
Isaiah 1:24Kwa hiyo Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, 2 Mwenye Nguvu wa Israeli, asema hivi: 1 “Lo, nitapata faraja kutoka kwa adui zangu 2 na kujilipizia kisasi juu ya watesi wangu. 1
Jeremiah 6:6Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: 1 “Kateni miti mjenge boma 2 kuzunguka Yerusalemu. 1 Mji huu ni lazima uadhibiwe, 2 umejazwa na uonevu. 1
Jeremiah 9:8Ndimi zao ni mshale wenye sumu, 2 hunena kwa udanganyifu. 1 Kwa kinywa chake kila mmoja huzungumza maneno mazuri na jirani yake, 2 lakini moyoni mwake humtegea mtego. 1
Jeremiah 23:2Kwa hiyo hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, analowaambia wachungaji wanaowachunga watu wangu: “Kwa sababu mmelitawanya kundi langu na kuwafukuzia mbali, wala hamkuwatunza, basi mimi nitawaadhibu kwa ajili ya uovu mliofanya,” asema Bwana.