Isaiah 64:11
Hekalu letu takatifu na tukufu, mahali ambapo baba zetu walikusifu wewe, 2 limechomwa kwa moto, 2 navyo vitu vyote tulivyovithamini vimeharibika. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
10Miji yako mitakatifu imekuwa jangwa; 2 hata Sayuni ni jangwa, Yerusalemu ni ukiwa. 1
12Ee Bwana, baada ya haya yote, utajizuia? 2 Je, utanyamaza kimya na kutuadhibu kupita kiasi?
Cross References
1 Kings 8:56“Ahimidiwe Bwana, aliyewapa pumziko watu wake Israeli kama vile alivyokuwa ameahidi. Hakuna hata neno moja lililopunguka kati ya ahadi zote nzuri alizozitoa kupitia mtumishi wake Mose.
2 Chronicles 6:4Kisha akasema: “Ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye kwa mikono yake mwenyewe ametimiza lile alilomwahidi Daudi baba yangu kwa kinywa chake mwenyewe. Kwa kuwa alisema,
2 Chronicles 7:6Makuhani wakasimama kwenye nafasi zao, vivyo hivyo Walawi wakiwa na vyombo vya uimbaji vya Bwana ambavyo Mfalme Daudi alikuwa ametengeneza kwa ajili ya kumsifu Bwana, navyo vilitumika wakati aliposhukuru, akisema, “Upendo wake wadumu milele.” Mkabala na Walawi, makuhani walipiga tarumbeta zao, nao Waisraeli wote walikuwa wamesimama.
2 Chronicles 36:19Wakalichoma Hekalu la Mungu na kuzibomoa kuta za Yerusalemu, wakachoma moto majumba yote ya kifalme na kuharibu kila kitu chake cha thamani.
Jeremiah 52:13Alichoma moto Hekalu la Bwana, jumba la kifalme, na nyumba zote za Yerusalemu. Aliteketeza kila jengo muhimu.
Lamentations 1:10Adui ametia mikono 2 juu ya hazina zake zote, 1 aliona mataifa ya kipagani 2 wakiingia mahali patakatifu pake, 1 wale uliowakataza kuingia 2 kwenye kusanyiko lako. 1