Yeremia 19:7
“ ‘Nitaiharibu mipango ya Yuda na Yerusalemu mahali hapa. Nitawafanya waanguke kwa upanga mbele ya adui zao, katika mikono ya wale watafutao uhai wao, nami nitaitoa mizoga yao kuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Leviticus 26:17Nitauelekeza uso wangu dhidi yenu ili mshindwe na adui zenu; wale wanaowachukia watawatawala, nanyi mtakimbia ingawa hakuna mtu anayewafukuza.
Deuteronomy 28:25Bwana atakufanya ushindwe mbele ya adui zako. Utawajia kwa njia moja lakini utawakimbia mbele yao kwa njia saba, nawe utakuwa kitu cha kuchukiza kwa falme zote za dunia.
2 Kings 21:14Nitawakataa mabaki wa urithi wangu na kuwatia mikononi mwa adui zao. Watapokonywa mali zao na kutekwa nyara na adui zao wote,
Psalms 33:10Bwana huzuia mipango ya mataifa, 2 hupinga makusudi ya mataifa. 1
Proverbs 21:30Hakuna hekima, wala akili, wala mpango 2 unaoweza kufaulu dhidi ya Bwana. 1
Isaiah 28:17Nitaifanya haki kuwa kamba ya kupimia 2 na uadilifu kuwa timazi; 1 mvua ya mawe itafagia kimbilio lenu, huo uongo, 2 nayo maji yatafurikia mahali penu pa kujificha. 1