Jeremiah 6:21
Kwa hiyo hivi ndivyo asemavyo Bwana: 1 “Nitaweka vikwazo mbele ya watu hawa. 2 Baba na wana wao watajikwaa juu yake, 2 majirani na marafiki wataangamia.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Isaiah 8:14naye atakuwa mahali patakatifu; 2 lakini kwa nyumba zote mbili za Israeli atakuwa 1 jiwe lile linalosababisha watu kujikwaa 2 na mwamba wa kuwaangusha. 1 Kwa watu wa Yerusalemu, 2 atakuwa mtego na tanzi. 1
Isaiah 9:14Kwa hiyo Bwana atakatilia mbali kutoka Israeli kichwa na mkia, 2 tawi la mtende na tete katika siku moja. 1
Jeremiah 9:21Mauti imeingia ndani kupitia madirishani, 2 imeingia kwenye majumba yetu ya fahari; 1 imewakatilia mbali watoto katika barabara 2 na vijana waume kutoka viwanja vya miji.
Jeremiah 15:2Nao kama wakikuuliza, ‘Twende wapi?’ Waambie, ‘Hili ndilo Bwana asemalo: 1 “ ‘Wale waliowekwa kwa ajili ya kufa, wakafe; 2 waliowekwa kwa ajili ya upanga, kwa upanga; 1 waliowekwa kwa ajili ya njaa, kwa njaa: 2 waliowekwa kwa ajili ya kutekwa, watekwe.’ ”
Jeremiah 18:21Kwa hiyo uwaache watoto wao waone njaa; 2 uwaache wauawe kwa makali ya upanga. 1 Wake zao wasiwe na watoto, na wawe wajane; 2 waume wao wauawe, 1 nao vijana wao waume 2 wachinjwe kwa upanga vitani. 1
Jeremiah 21:7Baada ya hayo, nitamtia Sedekia mfalme wa Yuda, maafisa wake na watu wa mji huu ambao walinusurika tauni, upanga na njaa, mkononi mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli, na kwa adui zao wale wanaotafuta uhai wao. Atawaua kwa upanga; hatakuwa na rehema juu yao au huruma wala kuwasikitikia,’ asema Bwana.