Ayubu 9:15
Ingawa sikuwa na hatia, sikuweza kumjibu; 2 ningeweza tu kumsihi Mhukumu wangu anihurumie. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
Whom, though I were righteous, yet would I not answer, but I would make supplication to my judge.
In Context
14“Ni vipi basi mimi nitaweza kubishana naye? 2 Nawezaje kupata maneno ya kuhojiana naye? 1
16Hata kama ningemwita kwenye shauri, naye akakubali, 2 siamini kama angenisikiliza. 1
Cross References
1 Kings 8:38wakati dua au maombi yatakapofanywa na mmojawapo wa watu wako Israeli, kila mmoja akitambua taabu za moyo wake mwenyewe, naye akainyoosha mikono yake kuelekea Hekalu hili:
Job 5:8“Lakini ingekuwa ni mimi, ningemlalamikia Mungu, 2 ningeliweka shauri langu mbele zake. 1
Job 10:2Nitamwambia Mungu: Usinihukumu, 2 bali niambie una mashtaka gani dhidi yangu. 1
Job 22:27Utamwomba yeye, naye atakusikia, 2 nawe utazitimiza nadhiri zako. 1
Job 34:31“Kama mwanadamu akimwambia Mungu, 2 ‘Nimekosa lakini sitatenda dhambi tena. 1
Daniel 9:3Kwa hiyo nikamgeukia Bwana Mungu na kumsihi katika maombi na dua, katika kufunga, na kuvaa nguo ya gunia na kujipaka majivu.