John 14:15
“Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
If ye love me, keep my commandments.
In Context
14Kama mkiniomba lolote kwa Jina langu nitalifanya. 1 Yesu Aahidi Roho Mtakatifu
16Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine akae nanyi milele.
Cross References
Matthew 10:37“Yeyote ampendaye baba yake au mama yake kuliko anavyonipenda mimi, hastahili kuwa wangu. Yeyote ampendaye mwanawe au binti yake kuliko anavyonipenda mimi, hastahili kuwa wangu.
John 8:42Yesu akawaambia, “Kama Mungu angekuwa Baba yenu, mngenipenda, kwa maana nilitoka kwa Mungu na sasa niko hapa. Sikuja kwa ajili yangu mwenyewe, ila yeye alinituma.
John 15:10Mkizishika amri zangu mtakaa katika pendo langu, kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.
1 Corinthians 16:22Kama mtu yeyote hampendi Bwana Yesu Kristo, na alaaniwe. Bwana wetu, njoo. + 16:22 Kwa Kiaramu ni Marana tha.
2 Corinthians 8:8Siwaamrishi, lakini nataka kujaribu unyofu wa upendo wenu kwa kuulinganisha na bidii ya wengine.
Ephesians 3:16Namwomba Mungu awaimarishe kwa kuwatia nguvu mioyo yenu kwa njia ya Roho wake kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake,