John 16:21
Mwanamke anapokuwa na utungu wa kuzaa huwa na maumivu kwa sababu saa yake imewadia. Lakini mtoto akiisha kuzaliwa, yule mwanamke husahau maumivu hayo kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtoto ulimwenguni.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 3:16Kwa mwanamke akasema, 1 “Nitakuzidishia sana utungu wakati wa kuzaa kwako; 2 kwa utungu utazaa watoto. 1 Tamaa yako itakuwa kwa mumeo 2 naye atakutawala.”
Genesis 30:23Akapata mimba na akamzaa mwana na kusema, “Mungu ameniondolea aibu yangu.”
Job 11:16Hakika utaisahau taabu yako, 2 utaikumbuka tu kama maji yaliyokwisha kupita. 1
Isaiah 13:8Hofu itawakamata, 2 uchungu na maumivu makali yatawashika, 1 watagaagaa kama mwanamke aliye na utungu wa kuzaa. 1 Watatazamana kwa hofu kila mtu na mwenzake, 2 nyuso zao zikiwaka kama moto. 1
Jeremiah 30:6Ulizeni na mkaone: 2 Je, mwanaume aweza kuzaa watoto? 1 Kwa nini basi ninaona kila mwanaume mwenye nguvu 2 ameweka mikono yake tumboni 1 kama mwanamke aliye na utungu wa kuzaa, 2 kila uso ukigeuka rangi kabisa? 1
Micah 4:10Gaagaa kwa utungu, ee Binti Sayuni, 2 kama mwanamke mwenye utungu wa kuzaa, 1 kwa kuwa sasa ni lazima uuache mji 2 ukapige kambi uwanjani. 1 Utakwenda Babeli; 2 huko utaokolewa. 1 Huko Bwana atakukomboa 2 kutoka mikononi mwa adui zako. 1