Waamuzi 17:3
Alipozirudisha zile shekeli 1,100 za fedha kwa mama yake, mama yake akamwambia, “Mimi nimeiweka fedha hii wakfu kwa Bwana kwa ajili ya mwanangu kutengenezea kinyago cha kuchonga na sanamu ya kusubu. Mimi nitakurudishia wewe.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 20:23Msijifanyizie miungu yoyote na kuilinganisha nami, msijitengenezee miungu ya fedha wala miungu ya dhahabu.
Leviticus 19:4“ ‘Msiabudu sanamu, wala msijitengenezee miungu ya shaba. Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.
Deuteronomy 27:15“Alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga au mwenye kusubu sanamu, kitu ambacho ni chukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi stadi, na kuisimamisha kwa siri.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”
Judges 18:5Kisha wakamwambia, “Tafadhali tuulizie kwa Mungu kama safari yetu itafanikiwa.”
Psalms 115:4Lakini sanamu zao ni za fedha na dhahabu, 2 zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu. 1
Isaiah 44:9Wote wachongao sanamu ni ubatili, 2 navyo vitu wanavyovithamini havifai kitu. 1 Wale ambao wanazitetea ni vipofu, 2 ni wajinga, nao waaibika. 1