Waamuzi 3:12
Waisraeli wakafanya maovu mbele za Bwana tena, kwa kuwa walifanya maovu hayo Bwana akamtia nguvu Egloni mfalme wa Moabu dhidi ya Israeli.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 9:16Lakini nimekuinua wewe kwa kusudi hili hasa, ili nipate kukuonyesha uwezo wangu, na ili Jina langu lipate kutangazwa duniani yote.
Judges 2:14Hivyo hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia mikononi mwa wavamizi waliowateka nyara. Akawauza katika mikono ya adui zao pande zote, hivyo hawakuweza tena kuwazuia adui zao.
1 Samuel 12:9“Lakini wakamsahau Bwana Mungu wao, hivyo Mungu akawauza katika mkono wa Sisera, jemadari wa jeshi la Hazori na katika mikono ya Wafilisti na mfalme wa Moabu, ambaye alipigana dhidi yao.
Isaiah 10:15Je, shoka laweza kujigamba kuwa na nguvu zaidi 2 kuliko yule anayelitumia, 1 au msumeno kujisifu 2 dhidi ya yule anayeutumia? 1 Ni kana kwamba fimbo ingeweza kumwinua yeye aichukuaye, 2 au mkongojo ungemwinua mwenye kuutumia! 1
Isaiah 45:1“Hili ndilo asemalo Bwana kwa mpakwa mafuta wake, 2 Koreshi, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume 1 kutiisha mataifa mbele yake 2 na kuwavua wafalme silaha zao, 1 kufungua milango mbele yake 2 ili malango yasije yakafungwa: 1
Daniel 4:22Ee mfalme, wewe ndiwe ule mti! Umekuwa mkubwa na mwenye nguvu, nao ukuu wako umekua mpaka kufika juu angani, nayo mamlaka yako yameenea mpaka miisho ya dunia.