Lamentations 2:11
Macho yangu yamedhoofika kwa kulia, 2 nina maumivu makali ndani, 1 moyo wangu umemiminwa ardhini 2 kwa sababu watu wangu wameangamizwa, 1 kwa sababu watoto na wanyonyao wanazimia 2 kwenye barabara za mji. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
1 Samuel 30:4Hivyo Daudi na watu wake wakapiga yowe mpaka wakaishiwa na nguvu za kulia.
Psalms 6:7Macho yangu yamedhoofika kwa kuhuzunika, 2 yamedhoofika kwa sababu ya adui zangu wote. 1
Psalms 31:9Ee Bwana unihurumie, kwa kuwa niko kwenye shida; 2 macho yangu yanafifia kwa huzuni, 2 nafsi yangu na mwili wangu kwa sikitiko. 1
Isaiah 22:4Kwa hiyo nilisema, “Geukia mbali nami, 2 niache nilie kwa uchungu. 1 Usijaribu kunifariji 2 juu ya maangamizi ya watu wangu.” 1
Isaiah 51:20Wana wako wamezimia, 2 wamelala kwenye mwanzo wa kila barabara, 2 kama swala aliyenaswa kwenye wavu. 1 Wamejazwa na ghadhabu ya Bwana 2 na makaripio ya Mungu wako. 1
Jeremiah 8:19Sikia kilio cha watu wangu 2 kutoka nchi ya mbali: 1 “Je, Bwana hayuko Sayuni? 2 Je, Mfalme wake hayuko tena huko?” 1 “Kwa nini wamenikasirisha kwa vinyago vyao, 2 kwa sanamu zao za kigeni zisizofaa?” 1