Walawi 26:16
ndipo nitakapowafanyia hili: Nitawaletea juu yenu hofu ya ghafula, magonjwa ya kufisha, na homa itakayopofusha macho yenu na kuwaondolea uhai wenu. Mtapanda mbegu bila mafanikio, kwa sababu adui zenu wataila.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Deuteronomy 28:21Bwana atakupiga kwa magonjwa mpaka akuangamize kutoka nchi unayoingia kuimiliki.
Deuteronomy 28:51Watakula wadogo wa mifugo yako na mazao ya nchi yako mpaka umeangamia. Hawatakuachia nafaka, divai mpya au mafuta, wala ndama wowote wa kundi lako au wana-kondoo wa kundi lako mpaka umekuwa magofu.
Deuteronomy 32:25Barabarani upanga utawakosesha watoto; 2 nyumbani mwao hofu itatawala. 1 Vijana wao wa kiume na wa kike wataangamia, 2 pia watoto wachanga na wazee wenye mvi. 1
Judges 6:11Malaika wa Bwana akaja akaketi chini ya mti wa mwaloni huko Ofra, ambao ulikuwa mali ya Yoashi, Mwabiezeri, ambako Gideoni mwanawe alikuwa akipepeta ngano penye shinikizo la kukamulia zabibu, ili kuificha Wamidiani wasiione.
Job 15:20Mtu mwovu siku zake zote hupata mateso, 2 miaka yote aliwekewa mkorofi. 1
Job 20:25Atauchomoa katika mgongo wake, 2 ncha ingʼaayo kutoka ini lake. 1 Vitisho vitakuja juu yake; 2