Luke 9:22
Yesu akasema, “Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi na kukataliwa na wazee, viongozi wa makuhani, na walimu wa sheria, na itampasa auawe, lakini siku ya tatu kufufuliwa kutoka mauti.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
21Yesu akawakataza wasimwambie mtu yeyote jambo hilo.
Cross References
Genesis 3:15Nami nitaweka uadui 2 kati yako na huyo mwanamke, 2 na kati ya uzao wako na wake, 1 yeye atakuponda kichwa, 2 nawe utamuuma kisigino.”
Psalms 69:1Ee Mungu, niokoe, 2 kwa maana maji yamenifika shingoni. 1
Daniel 9:26Baada ya majuma sitini na mawili, Mpakwa Mafuta atakatiliwa mbali, wala hatabaki na kitu. Watu wa mtawala atakayekuja watauharibu mji pamoja na mahali patakatifu. Mwisho utakuja kama mafuriko: Vita vitaendelea mpaka mwisho, nao ukiwa umeamriwa.
Matthew 16:21Tangu wakati huo, Yesu alianza kuwaeleza wanafunzi wake kwamba hana budi kwenda Yerusalemu na kupata mateso mengi mikononi mwa wazee, viongozi wa makuhani, na walimu wa sheria, na kwamba itampasa auawe lakini siku ya tatu kufufuliwa.
Matthew 17:22Siku moja walipokuwa pamoja huko Galilaya, Yesu akawaambia, “Mwana wa Adamu atasalitiwa na kutiwa mikononi mwa watu.
Mark 9:31kwa maana alikuwa anawafundisha wanafunzi wake. Akawaambia, “Mwana wa Adamu atasalitiwa na kutiwa mikononi mwa watu. Nao watamuua, lakini siku tatu baada ya kuuawa atafufuka.”