Matthew 11:23
Nawe Kapernaumu, je, utainuliwa hadi mbinguni? La hasha, utashushwa mpaka kuzimu. + 11:23 Kuzimu ni Mahali pa wafu. Miujiza iliyofanyika kwako ingefanyika huko Sodoma, mji huo ungalikuwepo hadi leo.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 13:13Basi watu wa Sodoma walikuwa waovu, wakifanya sana dhambi dhidi ya Bwana.
Isaiah 14:13Ulisema moyoni mwako, 2 “Nitapanda juu hadi mbinguni, 1 nitakiinua kiti changu cha enzi 2 juu ya nyota za Mungu, 1 nitaketi nimetawazwa 2 juu ya mlima wa kusanyiko, 2 kwenye vimo vya juu sana vya Mlima Mtakatifu. 1
Ezekiel 16:48Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, dada yako Sodoma pamoja na binti zake, kamwe hawakufanya yale ambayo wewe na binti zako mmefanya.
Ezekiel 31:16Niliyafanya mataifa yatetemeke kwa kishindo cha kuanguka kwake wakati nilipoushusha chini kaburini pamoja na wale washukao shimoni. Ndipo miti yote ya Edeni, miti iliyo bora kuliko yote na iliyo mizuri sana ya Lebanoni, miti yote ile iliyokunywa maji vizuri, ilifarijika hapa duniani.
Matthew 4:13Akaondoka Nazareti akaenda kuishi Kapernaumu, mji ulioko karibu na bahari, katika mipaka ya nchi ya Zabuloni na Naftali,
Matthew 16:18Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, hata malango ya Kuzimu hayataweza kulishinda.