Mathayo 28:9
Ghafula, Yesu akakutana nao, akasema, “Salamu!” Wale wanawake wakamkaribia, wakaishika miguu yake, wakamwabudu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Song of Solomon 3:3Walinzi walinikuta 2 walipokuwa wakizunguka mji. 1 Nikawauliza, “Je, mmemwona 2 yule moyo wangu umpendaye?” 1
Matthew 14:33Ndipo wote waliokuwa ndani ya ile mashua wakamwabudu Yesu, wakisema, “Hakika, wewe ndiwe Mwana wa Mungu.” 1 Yesu Awaponya Wagonjwa Genesareti (Marko 6:53-56)
Mark 16:9Yesu alipofufuka alfajiri na mapema siku ya kwanza ya juma alimtokea kwanza Maria Magdalene, yule ambaye alikuwa amemtoa pepo wachafu saba.
Luke 7:38Yule mwanamke akasimama nyuma ya miguu ya Yesu akilia. Akailowanisha miguu yake kwa machozi yake, kisha akaifuta kwa nywele zake, akaibusu na kuimiminia manukato.
John 12:3Kisha Maria akachukua chupa ya painti moja + 12:3 Painti moja ni kama nusu lita. yenye manukato ya nardo + 12:3 Nardo ni aina ya mafuta yaliyokuwa yanatengenezwa kutokana na mimea yenye mizizi inayotoa harufu nzuri. safi ya thamani kubwa, akayamimina miguuni mwa Yesu na kuifuta kwa nywele zake. Nyumba nzima ikajaa harufu nzuri ya manukato.
John 20:19Ikawa jioni ya ile siku ya kwanza ya juma, wanafunzi wake walikuwa pamoja, milango ikiwa imefungwa kwa kuwaogopa Wayahudi. Naye Yesu aliwatokea, akasimama katikati yao, akasema, “Amani iwe nanyi!”