Micah 1:7
Sanamu zake zote 2 zitavunjwa vipande vipande; 1 zawadi zake zote za Hekalu 2 zitachomwa kwa moto; 2 nitaharibu vinyago vyake vyote. 1 Kwa kuwa alikusanya zawadi zake 2 kutokana na ujira wa kahaba, 1 nazo zitatumika tena 2 kulipa mishahara ya kahaba.” 1 Kulia Na Kuomboleza 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Leviticus 26:30Nitapaharibu mahali penu pa juu pa kuabudia miungu, nibomoe madhabahu zenu za kufukizia uvumba, na kuzilundika maiti zenu juu ya sanamu zenu zisizo na uhai, nami nitawachukia ninyi sana.
Deuteronomy 23:18Kamwe usilete mapato ya ukahaba ikiwa ni ya mwanamke au ni ya mwanaume katika nyumba ya Bwana Mungu wako kwa ajili ya nadhiri yoyote, kwa sababu Bwana Mungu wako anachukizwa na yote mawili.
2 Chronicles 31:1Baada ya mambo haya yote kumalizika, Waisraeli ambao walikuwako huko wakaenda kwenye miji ya Yuda, wakayavunja yale mawe ya kuabudia na kuzikatakata zile nguzo za Ashera. Wakabomoa mahali pa juu pa kuabudia miungu pamoja na madhabahu zake kila mahali katika Yuda na Benyamini na katika Efraimu na Manase. Baada ya kuviharibu hivi vyote, Waisraeli wakarudi katika miji yao wenyewe na kwenye milki zao.
Isaiah 27:9Kwa hili, basi, hatia ya Yakobo itafanyiwa upatanisho, 2 nalo hili litakuwa matunda ya utimilizo wa kuondolewa kwa dhambi yake: 1 Wakati atakapoyafanya mawe yote ya madhabahu 2 kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa vipande vipande, 1 hakuna nguzo za Ashera au madhabahu za kufukizia uvumba 2 zitakazobaki zimesimama. 1
Ezekiel 6:6Popote mnapoishi, miji hiyo itafanywa ukiwa na mahali pa juu pa kuabudia miungu patabomolewa, ili madhabahu yenu ifanywe ukiwa na kuharibiwa, sanamu zenu zitavunjavunjwa na kuharibiwa, madhabahu yenu ya kufukizia uvumba yatabomolewa na kila mlichokifanya kitakatiliwa mbali.
Hosea 2:12Nitaiharibu mizabibu yake na mitini yake, 2 ambayo alisema yalikuwa malipo yake 2 kutoka kwa wapenzi wake; 1 nitaifanya kuwa kichaka, 2 nao wanyama pori wataila. 1