Micah 5:2
“Lakini wewe, Bethlehemu Efrathi, 2 ingawa u mdogo miongoni mwa koo za Yuda, 1 kutoka kwako atatokea kwa ajili yangu 2 yeye atakayekuwa mtawala katika Israeli, 1 ambaye asili yake ni kutoka zamani, 2 kutoka milele.” 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 35:19Kwa hiyo Raheli akafa, akazikwa kando ya njia iendayo Efrathi (ndio Bethlehemu).
Genesis 49:10Fimbo ya ufalme haitaondoka kwa Yuda, 2 wala fimbo ya mtawala kati ya miguu yake, 1 hadi aje yeye ambaye milki ni yake, 2 ambaye utii wa mataifa ni wake. 1
Exodus 18:25Mose akawachagua watu wenye uwezo kutoka Israeli yote, akawafanya kuwa viongozi wa watu, maafisa juu ya maelfu, mamia, hamsini na makumi.
Judges 17:7Basi palikuwa na kijana mmoja wa Bethlehemu ya Yuda. Yeye alikuwa Mlawi aliyeishi miongoni mwa kabila la Yuda.
1 Samuel 8:12Baadhi yao atawaweka kuwa majemadari wa jeshi wa maelfu na majemadari wa jeshi wa hamsini, wengine kulima mashamba yake na kuvuna mavuno yake, pia na wengine kutengeneza silaha za vita na vifaa kwa ajili ya magari yake.
1 Samuel 17:12Basi Daudi alikuwa mwana wa Mwefrathi jina lake Yese aliyekuwa ametoka Bethlehemu ya Yuda. Yese alikuwa na wana wanane, naye wakati wa Sauli alikuwa mzee tena wa umri mkubwa.