Micah 7:18
Ni nani Mungu kama wewe, 2 ambaye anaachilia dhambi 1 na kusamehe makosa 2 ya mabaki ya urithi wake? 1 Wewe huwi na hasira milele, 2 bali unafurahia kuonyesha rehema. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 33:18Kisha Mose akasema, “Basi nionyeshe utukufu wako.”
Exodus 34:9Mose akasema, “Ee Bwana, kama nimepata kibali mbele zako, basi Bwana uende pamoja nasi. Ingawa watu hawa ni wenye shingo ngumu, samehe uovu wetu na dhambi yetu, tuchukue kuwa urithi wako.” 1 Kufanya Agano Upya (Kutoka 23:14-19; Kumbukumbu 7:1-5; 16:1-17)
Numbers 23:21“Haijaonekana bahati mbaya katika Yakobo, 2 wala taabu katika Israeli. 1 Bwana, Mungu wao yu pamoja nao, 2 nayo sauti kuu ya Mfalme imo katikati yao. 1
Judges 10:16Nao wakaiondoa hiyo miungu migeni katikati yao nao wakamtumikia Bwana. Naye akahuzunika kwa sababu ya taabu ya Israeli.
Nehemiah 9:17Wakakataa kusikiliza na kushindwa kukumbuka miujiza uliyoifanya miongoni mwao. Wakawa na shingo ngumu, na katika uasi wao wakamchagua kiongozi ili warudi kwenye utumwa wao. Lakini wewe ni Mungu mwenye kusamehe, mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo. Kwa hiyo hukuwaacha,
Psalms 65:3Tulipokuwa tumefunikwa kabisa na dhambi, 2 wewe ulisamehe makosa yetu. 1