Proverbs 11:6
Haki ya wanyofu huwaokoa, 2 bali wasio waaminifu hunaswa na tamaa mbaya. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 30:33Uadilifu wangu utanishuhudia siku zijazo, kila utakapochunguza ujira ambao umenilipa mimi. Mbuzi yeyote wangu ambaye hana mabakabaka wala madoadoa, au mwana-kondoo ambaye si mweusi, atahesabika ameibwa.”
1 Samuel 12:3Mimi ninasimama hapa. Shuhudieni juu yangu mbele za Bwana na mpakwa mafuta wake. Nimechukua maksai wa nani? Nimechukua punda wa nani? Ni nani nimepata kumdanganya? Ni nani nimepata kumwonea? Ni kutoka kwenye mkono wa nani nimepokea rushwa ili kunifanya nifumbe macho yangu? Kama nimefanya chochote katika hivi, mimi nitawarudishia.”
1 Kings 2:44Pia mfalme akamwambia Shimei, “Unajua katika moyo wako makosa uliyomtendea baba yangu Daudi. Sasa Bwana atakulipiza kwa ajili ya mabaya yako uliyotenda.
Proverbs 5:22Matendo mabaya ya mtu mwovu humnasa yeye mwenyewe; 2 kamba za dhambi yake humkamata kwa nguvu. 1