Proverbs 2:6
Kwa maana Bwana hutoa hekima, 2 na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
For the LORD giveth wisdom: out of his mouth cometh knowledge and understanding.
In Context
5ndipo utakapoelewa kumcha Bwana 2 na kupata maarifa ya Mungu. 1
7Anahifadhi ushindi kwa ajili ya mwadilifu, 2 yeye ni ngao kwa wale wasio na lawama, 1
Cross References
Exodus 31:3nami nimemjaza Roho wa Mungu, pamoja na ustadi, uwezo na ujuzi katika aina zote za ufundi,
1 Kings 3:12nitafanya lile uliloomba. Nitakupa moyo wa hekima na wa ufahamu, kiasi kwamba hajakuwepo mtu mwingine kama wewe, wala kamwe hatakuwepo baada yako.
1 Kings 10:24Dunia yote ikatafuta kukutana na Solomoni ili kusikia hekima ambayo Mungu alikuwa ameiweka katika moyo wake.
Ezra 7:25Nawe Ezra, kufuatana na hekima ya Mungu wenu uliyo nayo, weka mahakimu na waamuzi wote wanaozifahamu sheria za Mungu wenu ili watoe haki kwa watu wote wa Ngʼambo ya Mto Frati. Nawe inakupasa umfundishe yeyote ambaye hazifahamu.
Job 12:16Kwake kuna nguvu na ushindi; 2 adanganywaye na adanganyaye, wote wawili ni wake. 1
Psalms 19:7Sheria ya Bwana ni kamilifu, 2 ikihuisha nafsi. 1 Shuhuda za Bwana ni za kuaminika, 2 zikimpa mjinga hekima. 1