Romans 3:20
Kwa hiyo hakuna binadamu hata mmoja atakayehesabiwa haki mbele za Mungu kwa matendo ya sheria, kwa maana sheria hutufanya tuitambue dhambi. 1 Haki Kwa Njia Ya Imani
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Job 25:4Mtu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu? 2 Awezaje mtu aliyezaliwa na mwanamke kuwa safi? 1
Psalms 143:2Usimhukumu mtumishi wako, 2 kwa kuwa hakuna mtu anayeishi aliye mwenye haki mbele zako. 1
Romans 2:13Kwa maana si wale wanaoisikia sheria ambao ni wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale wanaoitii sheria ndio watakaohesabiwa haki.
Romans 4:13Kwa maana ile ahadi kwamba angeurithi ulimwengu haikuja kwa Abrahamu au kwa wazao wake kwa njia ya sheria bali kwa njia ya haki ipatikanayo kwa imani.
Romans 5:13kwa maana kabla sheria haijatolewa, dhambi ilikuwepo ulimwenguni. Lakini dhambi haihesabiwi wakati hakuna sheria.
Romans 7:7Tuseme nini basi? Kwamba sheria ni dhambi? La, hasha! Lakini, isingekuwa kwa sababu ya sheria, nisingalijua dhambi. Nisingalijua kutamani ni nini kama sheria haikusema, “Usitamani.”