2 Nyakati 14:11
Kisha Asa akamlilia Bwana Mungu wake na kusema, “Ee Bwana, hakuna yeyote aliye kama wewe wa kuwasaidia wasio na nguvu dhidi ya wenye nguvu. Utusaidie, Ee Bwana, wewe ndiwe Mungu wetu, kwa kuwa tunakutumainia wewe, nasi kwa jina lako tumekuja dhidi ya jeshi hili kubwa. Ee Bwana, wewe ndiwe Mungu wetu, usiwaache wanadamu wakushinde wewe.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
10Asa akatoka kumkabili, nao wakapanga vita katika Bonde la Sefatha karibu na Maresha.
12Bwana akawapiga Wakushi mbele ya Asa na Yuda. Wakushi wakakimbia,
Cross References
Exodus 14:10Farao alipokaribia, Waisraeli wakainua macho yao, wakawaona Wamisri wakija nyuma yao. Wakashikwa na hofu, wakamlilia Bwana.
Deuteronomy 32:27Lakini nilihofia dhihaka za adui, 2 adui asije akashindwa kuelewa, 1 na kusema, ‘Mikono yetu imeshinda; 2 Bwana hakufanya yote haya.’ ” 1
Deuteronomy 32:36Bwana atawahukumu watu wake, 2 na kuwahurumia watumishi wake 1 atakapoona nguvu zao zimekwisha 2 wala hakuna yeyote aliyebaki, 2 mtumwa au aliye huru. 1
Judges 7:7Bwana akamwambia Gideoni, “Kwa hao watu 300 walioramba maji nitawaokoa ninyi, nami nitawatia Wamidiani mkononi mwako. Waache hao watu wengine wote warudi kila mmoja nyumbani mwake.”
1 Samuel 14:6Yonathani akamwambia kijana wake mbeba silaha, “Njoo, tuvukie doria ya wale jamaa wasiotahiriwa. Huenda Bwana atatenda kwa ajili yetu. Hakuna chochote kitakachoweza kumzuia Bwana kuokoa, kwamba ni kwa wingi au kwa uchache.”
1 Samuel 17:45Daudi akamwambia yule Mfilisti. “Wewe unanijia na upanga, mkuki na fumo, lakini mimi ninakujia kwa jina la Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa majeshi ya Israeli, ambaye wewe umemtukana.