Daniel 11:10
Wana wa mfalme wa Kaskazini watajiandaa kwa vita na kukusanya jeshi kubwa, ambalo litafagia nchi kama mafuriko yasiyozuilika na kuendelea na vita hadi kwenye ngome ya mfalme wa Kusini.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Isaiah 8:7kwa hiyo Bwana yu karibu kuleta dhidi yao 2 mafuriko makubwa ya Mto: + 8:7 Yaani Frati. 2 yaani mfalme wa Ashuru na fahari yake yote. 1 Yatafurika juu ya mifereji yake yote, 2 yatamwagikia juu ya kingo zake zote, 1
Jeremiah 46:7“Ni nani huyu ajiinuaye kama Mto Naili, 2 kama mito yenye maji yanayofanya mawimbi? 1
Daniel 9:26Baada ya majuma sitini na mawili, Mpakwa Mafuta atakatiliwa mbali, wala hatabaki na kitu. Watu wa mtawala atakayekuja watauharibu mji pamoja na mahali patakatifu. Mwisho utakuja kama mafuriko: Vita vitaendelea mpaka mwisho, nao ukiwa umeamriwa.
Daniel 11:22Ndipo jeshi kubwa litafagiliwa mbele yake; jeshi pamoja na mkuu mmoja wa agano wataangamizwa.
Daniel 11:39Atashambulia ngome zenye nguvu mno kwa msaada wa mungu wa kigeni naye atawaheshimu sana wale watakaomkubali yeye. Atawafanya watawala juu ya watu wengi, na atagawa nchi kwa gharama.