Daniel 8:13
Kisha nikamsikia mtakatifu mmoja akizungumza na mtakatifu mwingine, akamwambia, “Je, itachukua muda gani maono haya yatimie: maono kuhusu dhabihu ya kila siku, uasi unaosababisha ukiwa, kutwaliwa kwa mahali patakatifu, na jeshi litakalokanyagwa chini ya nyayo?”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
14Akaniambia, “Itachukua siku 2,300. Ndipo mahali patakatifu patawekwa wakfu tena.” 1 Tafsiri Ya Maono
Cross References
Judges 13:18Akamjibu, “Kwa nini unauliza Jina langu? Ni Jina la ajabu.”
Psalms 79:5Hata lini, Ee Bwana? Je, wewe utakasirika milele? 2 Wivu wako utawaka kama moto hadi lini? 1
Isaiah 9:6Kwa maana, kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, 2 tumepewa mtoto mwanaume, 2 nao utawala utakuwa mabegani mwake. 1 Naye ataitwa 2 Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, 2 Baba wa Milele, Mfalme wa Amani. 1
Daniel 4:10Haya ndiyo maono niliyoona nilipokuwa nimelala kitandani mwangu: Nilitazama, na mbele yangu ulisimama mti katikati ya nchi. Ulikuwa mrefu sana.
Daniel 4:23“Ee mfalme, wewe ulimwona mlinzi, aliye mtakatifu, akishuka kutoka mbinguni na kusema, ‘Ukateni mti na kuuangamiza, lakini kiacheni kisiki kikiwa kimefungwa kwa chuma na kwa shaba, kwenye majani ya kondeni, wakati mizizi yake inabaki ardhini. Mwacheni aloweshwe na umande wa mbinguni, mwacheni aishi kama wanyama pori mpaka nyakati saba zipite juu yake.’
Daniel 7:23“Alinipa maelezo haya: ‘Mnyama wa nne ni ufalme wa nne ambao utatokea duniani. Utakuwa tofauti na falme nyingine zote, nao utaharibu dunia nzima, ukiikanyaga chini na kuipondaponda.