Mhubiri 2:18
Nikachukia kila kitu nilichokuwa nimetaabikia chini ya jua, kwa sababu ni lazima nimwachie yule ajaye baada yangu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Psalms 17:14Ee Bwana, mkono wako uniokoe na watu wa jinsi hii, 2 kutokana na watu wa ulimwengu huu 2 ambao fungu lao liko katika maisha haya. 1 Na wapate adhabu ya kuwatosha. 2 Watoto wao na wapate zaidi ya hayo, 2 hukumu na iendelee kwa watoto wa watoto wao. 1
Psalms 49:10Wote wanaona kwamba watu wenye hekima hufa; 2 wajinga na wapumbavu vivyo hivyo huangamia 2 na kuwaachia wengine mali zao. 1
Ecclesiastes 1:13Nilitumia muda wangu wote kujifunza na kuvumbua kwa hekima yote yanayofanyika chini ya mbingu. Jinsi gani Mungu ameweka mzigo mzito juu ya wanadamu!
Ecclesiastes 2:26Kwa yule mtu anayempendeza Mungu, Mungu humpa hekima, maarifa na furaha, bali kwa mwenye dhambi Mungu humpa kazi ya kukusanya na kuhifadhi utajiri ili Mungu ampe yule anayempenda. Hili nalo pia ni ubatili, ni kukimbiza upepo.
Ecclesiastes 5:13Nimeshaona uovu mzito chini ya jua: 1 Utajiri uliolimbikizwa kwa kujinyima 2 na kuleta madhara kwa mwenye mali, 1
Ecclesiastes 9:9Furahia maisha na mke wako, umpendaye, siku zote za maisha ya ubatili uliyopewa na Mungu chini ya jua, siku zote za ubatili. Kwa maana hili ndilo fungu lako katika maisha na katika kazi yako ya taabu chini ya jua.