Genesis 7:23
Kila kitu chenye uhai juu ya uso wa nchi kilifutiliwa mbali, watu, wanyama, viumbe vitambaavyo na ndege warukao angani wakafutiliwa mbali toka duniani. Waliobaki ni Noa peke yake na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
22Kila kiumbe juu ya nchi kavu chenye pumzi ya uhai kikafa.
24Maji yakaifunika dunia kwa siku 150.
Cross References
Genesis 7:21Kila kiumbe hai kitambaacho juu ya nchi kikaangamia: Ndege, wanyama wa kufugwa, wanyama pori, viumbe vyote juu ya nchi na wanadamu wote.
Exodus 14:28Maji yakarudiana na kuyafunika magari ya vita na wapanda farasi pamoja na jeshi lote la Farao lililokuwa limewafuata Waisraeli ndani ya bahari. Hakuna hata mmoja wao aliyenusurika.
Job 22:15Je, utaifuata njia ya zamani, 2 ambayo watu waovu waliikanyaga? 1
Psalms 91:7Ijapo watu elfu wataangukia kando yako, 2 kumi elfu mkono wako wa kuume, 2 lakini haitakukaribia wewe. 1
Proverbs 11:4Utajiri haufaidi kitu katika siku ya ghadhabu, 2 bali haki huokoa kutoka mautini. 1
Ezekiel 14:14hata kama watu hawa watatu: Noa, Danieli na Ayubu wangekuwa ndani ya nchi hiyo, ndio hao tu wangeweza kujiokoa wenyewe kwa uadilifu wao, asema Bwana Mwenyezi.