Hagai 2:22
Nitapindua viti vya enzi vya falme, na kuziharibu kabisa nguvu za falme za kigeni. Nitapindua magari ya vita pamoja na waendeshaji wake; farasi na wapanda farasi wataanguka, kila mmoja kwa upanga wa ndugu yake.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
21“Mwambie Zerubabeli mtawala wa Yuda kwamba nitazitikisa mbingu na nchi.
Cross References
Exodus 14:17Nitaifanya mioyo ya Wamisri kuwa migumu kusudi waingie baharini wakiwafuatia. Nami nitajipatia utukufu kupitia Farao pamoja na jeshi lake lote, kupitia magari yake ya vita na wapanda farasi wake.
Exodus 15:4Magari ya vita ya Farao na jeshi lake 2 amewatosa baharini. 1 Maafisa wa Farao walio bora sana 2 wamezamishwa katika Bahari ya Shamu. 1
Judges 7:22Walipozipiga zile tarumbeta 300, Bwana akafanya watu katika kambi yote kugeuziana upanga kila mmoja na mwenziwe. Jeshi likakimbia mpaka Beth-Shita kuelekea Serera + 7:22 Au: Seretha. hadi mpakani mwa Abel-Mehola karibu na Tabathi.
2 Chronicles 15:6Taifa moja lilipigana na taifa lingine na mji mmoja ukapigana na mji mwingine, kwa sababu Mungu alikuwa anawahangaisha kwa taabu za kila aina.
Psalms 46:9Anakomesha vita hata miisho ya dunia, 2 anakata upinde na kuvunjavunja mkuki, 2 anateketeza ngao kwa moto. 1
Isaiah 9:19Kwa hasira ya Bwana Mwenye Nguvu Zote 2 nchi itachomwa kwa moto, 1 nao watu watakuwa kuni za kuchochea moto. 2 Hakuna mtu atakayemhurumia ndugu yake. 1